Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa PROF.Riziki Shemdoe amewataka walimu wapya kuripoti kwenye maeneo yao ya kazi kabla ya tarehe 14 Mwezi huu wa saba 2021.
Akizunguza na waandishi wa habari katika ziara ya kukagua shughuli za ukarabati wa madarasa pamoja na mabweni katika shule ya wasichana Iringa, iliyo gharimu zaidi ya shilingi milioni mia saba za kitanzania (TZS 700,000,000)
Prof. Shemdoe amesema kuwa waajiriwa wapya wasiporipoti kwa wakati katika vituo vyao vya kazi nafasi zao zitachukuliwa.
Aidha prof. Shemdoe amempongeza Katibu Tawala Mkoa Bi. Happiness Seneda na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu kwa usimamizi mzuri waliofanya katika ukarabati huo na pia amewataka wakurugenzi wote Nchini kuwasaidia watumishi wapya ikiwa ni pamoja na kuwakopesha fedha kwa ajili ya kujikim wakati wakijiandaa kupokea mishahara.
Kadhalika Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi.Blandina Nkondola ameelezea changamoto zilizopo ni upungufu wa walimu wa Elimu maalum,upungufu wa bweni moja na madarasa mawili pamoja na fedha kwa ajili ya umalizaji wa uzio.
Licha ya Mwalimu Mkuu kuelezea changamoto hizo katibu mkuu amehaidi kuzitatua kwa haraka ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni kumi (TZS 10,000,000) kiasi ambacho kilichoahidiwa na ofisi yake mapema mwaka huu
Bi.Maria Nicholaus ni miongoni mwa walimu waajiriwa wapya waliofika katika vituo vyao vya kazi mapema ameeleza namna alivopokelewa vizuri na kuahidi kufanya kazi kwa weledi katika kituo chake kipya cha kazi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa