Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Ndugu Happiness Seneda ameitaka Menejimenti ya Manispaa ya Iringa kuweka mikakati madhubuti ili kuhakikisha shughuli zote za Manispaa zinafanyika kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuzingatia ubora na kukamilisha kwa wakati uliopangwa.
Ndugu Seneda ameyasema hayo leo tarehe 24/6/2022 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ikiwa ni kikao kazi cha kujipima,kujisahihisha
na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji kazi ili Manispaa iweze kusonga mbele na kutoa huduma bora kwa wanachi na kuleta maendeleo kwa jamii .
Aidha Ndugu Seneda ameipongeza Menejimenti ya Manispaa ya Iringa kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha
2021/2022 kwa kukusanya shilingi bilioni 4.6 sawa na asilimia 95 ya lengo walilojiwekea kukusanya
Pia ameitaka Menejimenti kubuni vyanzo vipya vya mapato ili Manispaa ikusanye mapato zaidi.
Katika kikao kazi hicho wakuu wa idara na vitengo walipata fursa ya kuelezea mikakati waliyonayo kuboresha utendaji kazi katika kila Idara.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndugu Gerald Mwamuhamila amesema ameyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Katibu Tawala na kuahidi kuyafanyia kazi mara moja.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa