Katibu Tawala wa wilaya ya Iringa Ndugu Hashim Komba amewataka wazazi na walimu kuwafundisha wanafunzi uzalendo wa Nchi yao ili kujenga taifa lenye umoja ,upendo na mshikamano .
Ndugu hashim Komba metoa wito huo katika siku ya maadhimisho ya kumuenzi baba wa taifa hayati Julius Kambarage Nyerere yaliyofanyika shule ya kihesa secondary ambapo pia amewataka wazazi kuwalea wanafunzi kwa kufuata mienendo ya Baba wa Taifa
Aidha Ndugu Komba amesisitiza walimu kutosahau wajibu wao wa kuwahamasisha na kuwafunza umoja, mshikamano, upendo ,amani na kueleza mema ya nchi na kutopandikiza chuki kwa wanafunzi dhidi ya serikali iliyopo madarakani.
Maadhimisho hayo yameongozwa na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa madiwani ,Naibu Meya wa mamwenyekiti wa vijana uvvcm,katibu wa vijana uvvcm ,mwenyekiti wa baraza la ujamaa Tanzania bawata nao wamesisitiza kuhakikisha kuwakunbusha na kuchochea kumjenga kuwa kijana bora katik taifa letu
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa