“Nimpongeze Mkurugenzi pamoja na Wataalam wa Manispaa ya Iringa kwa kuanzisha Mradi wa Ufyatuaji wa tofali, kukarabati gari la taka pia ni muhimu kununua magari ya taka katika Manispaa yetu ili tuendelee kushika nafasi nzuri ya usafi”
Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Richard Kasesela katika Kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC) cha kupitia mapendekezo ya mpango wa bajeti ya Mwaka wa fedha 2020/2021 kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa Tarehe 24.1.2020.
Aidha kikao hicho kilikua na Agenda tano ikiwemo kusoma makadilio ya mapato na matumizi kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 na mpango wa bajeti wa Mwaka wa fedha 2020/2021.
Mbali na hapo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Richard Kasesela ,Kamati ya Usalama na Wataalam wamefanya Ziara katika stendi ya Kisasa ya Mabasi ya Igumbilo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa