“Tumekaa na kuzungumza na kuweka makubaliano na TANROAD kuhusu ujenzi wa wa barabara ya kutoka Iringa Mjini kuelekea Mbuga yetu ya Taifa ya Ruaha yenye kilomita 104 abayo hivi karibuni itaanza kujengwa”
Hayo yamesemwa leo Mei 26, 2022 na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada katika kikao cha Baraza la Madiwani la kupokea taarifa za kata kwa robo ya nne 2020/2021, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa
Sambamba na hilo Mhe. Ibrahim Ngwada amesema, wameingia makubaliano na TANROAD kuanza kujenga ‘TERMINAL BUILDING’ katika ujenzi wa awamu ya pili ya uwanja wa ndege wa Nduli na kusema kuwa tayari fedha za ujenzi huo zimeshafika
“Mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara hii pamoja na uwanja wetu wa ndege wa Nduli, vitakwenda kusisimua shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo shughuli za utalii na kilimo, katika Mkoa huu hususani hapa Manispaa ya Iringa kwani ndio Mjini” Mhe. Ngwada alisema .
Aidha katika kikao hicho, Baraza la Madiwani limempongeza Ndg.Mohamed Mtopa Mkuu wa Idara ya usafi na Mazingira kwa jitihada anazozionesha katika kuhakikisha Manispaa inaonekana safi muda wote.
Mhe. Eliud Mvela alichangia kwa kusema hayo katika kipindi cha maswali na majibu alipokaribishwa wakati wa uwasilishwaji wa taarifa hizo za utekelezaji za shughuli zinazofanyika kila kata.
Akihitimisha kikao hicho Mhe. Ngwada amemtaka Mkurugenzi kuhakikisha anazichukulia hatua changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na Madiwani katika kila taarifa walizoziwasilisha huku akiwataka pia watendaji wa Kata kuhakikisha wanafanya mikutano ya hadhara kwenye maeneo yao na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayotekelezwa kuanzia ngazi ya mitaa, kata, Halmashauri hadi kitaifa hali itakayowafanya wananchi kutambua na kushiriki vyema katika ujenzi wa Tanzania ya kisasa na yenye maendeleo madhubuti.
Gerald Mwamuhamila ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa amewashukuru wajumbe wa Baraza la Madiwani kwa ushirikiano uliopo baina yao na wataalam wa Manispaa katika kutekeleza majukumu ya kila siku na kuahidi atazifanyia kazi changamoto zote zilizobainishwa na Madiwani katika maeneo yao.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa