“Kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Iringa kunaboresha miradi, kutatua changamoto zinazojitokeza, kushauri na pale penye mapungufu kamati husika inashauri na mala moja utekelezaji unafanyika.”
Hayo yamebainika baada ya Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu inayoongozwa na Mheshimiwa Rhaphaeli Ngulo Diwani wa Kata ya Makorongoni kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Kamati hiyo, kutembelea na kushauri baadhi ya utekelezaji wa miradi ambapo ushauri unatekelezwa kwa maendeleo ya wananchi wa Manispaa ya Iringa.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na kukagua maendeleo ya Sifa- Saccos iliyopo Kata ya Gangilonga, Kihesa,kituo cha Afya Ngome ili kuona mwitikio wa huduma ya tiba kwa kadi (TIKA), Nduli wamekagua Ujenzi wa Madarasa ya Sekondari Nduli sambamba na mapokeo ya Kidato cha kwanza, Mtwivila kamati imekagua ukarabati wa Bwalo na jiko shule ya Msingi viziwi. Mkwawa kamati imetembelea Mashamba ya mfano yanayolima mbogamboga (green house).
Aidha Mh. Dady Igogo ameipongeza kamati kwa kufanya kazi bila kuangalia itikadi ya vyama vya siasa bali ni kujali maendeleo ya Wananchi wa Manispaa ya Iringa, naye Mwenyekiti wa kamati hiyo ameahidi kutatua changamoto ambazo zimeoneka katika ukaguzi wa Miradi ya maendeleo iliyokaguliwa na kamati hiyo kwa haraka,.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa