Maafisa Elimu na wakaguzi wa elimu katika Manispaa ya Iringa wametakiwa kutoka maofisini na kwenda mashuleni kukagua shule na maendeleo ya wanafunzi ili kusimamia ufaulu na miradi ya maendeleo kwani kwa kufanya hivi ufaulu utaongezeka na miradi ya maendeleo itatekelezeka kwa ufanisi mkubwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi , Afya na Elimu Mheshimiwa Raphael Ngullo alipokuwa akifunga kikao cha ziara ya kamati hiyo kutembelea miradi sita ya maendeleo KATIKA Manispaa YA Iringa.
“Ufaulu unaweza kuongezeka kutoka hapa tulipo na kufanya vizuri zaidi, lakini hili litawezekana kama tutatoka maofisini na kutembelea shule mala kwa mala.” Amesema Ngullo.
Katika ziara hiyo jumla ya miradi ya maendeleo sita ilitembelewa na kamati hiyo ukiwemo mradi wa soko la ngome ambalo ujenzi wake umekamilika na linatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni. Soko hilo la ngome lipo katika kata ya kihesa na kuna jumla ya meza 52 za ndani ya soko, na nje ya soko kunatarajiwa kujengwa meza nyingine za muda kuzunguka soko hilo.
Aidha kamati imetembelea na kukagua ujenzi wa vyoo 24 katika shule ya msingi Umoja ambapo ujenzi wa vyoo hivyo unatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi milioni 10,945,000/=. Akisoma taarifa mbele ya kamati hiyo mwalimu mkuu wa shule ya Umoja ndugu, Hawa Kaduma amesema ujenzi wa vyoo hivyo unafadhiliwa na shirika la UNDP,chini ya mkandarasi James Mvili.
Katika kuhakikisha fedha zinazopokelewa kutoka serikali kuu zinafanya kile kinachotarajiwa na kwa kuzingatia ubora kamati imekagua ujenzi wa darasa moja la P4R katika shule ya sekondari Mlandege ambapo darasa hilo limekamilika na limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 21,000,000/-, ikijumuisha gharama za ujenzi na uwekaji wa meza na viti.
Jumla ya miradi sita imetambelewa na kamati ukiwemo mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya sekondar Iringa wasichana, yanayojengwa na wadau CRDB,ujenzi wa soko la Ngome, kutembelea na kukagua ujenzi wa vyoo shule ya msingi Umoja, ujenzi wa madarasa shule ya msingi Njia Panda,ujenzi wa darasa shule ya sekondari Mlandege na ujenzi wa Maabara mbili shule ya sekondari Ipogolo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa