Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy ametoa siku saba kuanzia Septemba 5 mpaka 11, 2023 kwa machinga wote ambao wanafanya biashara katika maeneo yasio rasmi kuhamia maeneo yaliyorasimishwa na serikali.
Ametoa tamko hilo katika Mkutano wa Machinga uliofanyika katika Ukumbi wa Mercy Hall Jumanne Septemba 5 mwaka huu wakati akiwasihii machinga kufanya biashara katika maeneo yaliyo rasmi kwani serikali imetenga maeneo hayo kwa maslahi yao na wananchi.
“Machinga mfuate sheria na sio kugoma bali matatizo yenu yote yafikishwe mezani na kutafutiwa utatuzi kwa kufuata miongozo iliyoletwa na serikali ili muweze kufaidika kwa mambo mengi ikiwemo mifuko rasmi ya fedha kwaajili kukopeshwa machinga” Amesema Kessy
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya amesisitiza zoezi hilo kuanza mara moja kwani sheria hazita muacha yeyote atakayefanya biashara katika eneo lisilo rasmi, na pia ameuomba Uongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Taifa (SHIUMA) kubaki Mkoani hapo mpaka pale hali itakapo tulia ili iwe mfano kwa Taifa.
Aidha Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Mara Bw. Charles Waitara amewashauri machinga wa Mkoa wa Iringa kushikiriana na kushikamana kwani fursa nyingi zinawapita pasipo kujua;
“Machinga hawapati fursa kwasababu hawapo pamoja kwa maana wengine wapo maeneo rasmi na wengine hawapo maeneo rasmi, kitu kinachopelekea fursa nyingi kuwapita, mkishikamana na kushirikina kila mmoja atanufaika na fursa zilizopo huku tukiendelea kudumisha amani, umoja na utulivu” Amesema Waitara
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa