Madiwani wa Chama cha Mapinduzi Ccm,Leo wameapa kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo 2020 hadi 2025 mara baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika 0ktoba mwaka huu.
Zoezi hilo la kuapa limefanyka leo 10/12/2020 katika ukumbi wa Manispaa kwenye baraza la kwanza la madiwanina kushuhudiwa na umati mkubwa wa wananchi wa Manispaa ya Iringa ambapo mh.Meya wa Manispaa Ibrahim Ngwada na Naibu Meya Mh Kenyata likotiko wameshinda kwa kishindo kwa kila mmoja kupata kura zote 25 zilizopigwa.
Akifungua kikao hicho Mh.Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amewataka watumishi kutekeleza majukumu yao bila hofu yeyote na kuwa yeye na baraza zima la Madiwani hawatawaonea watumishi wala kufanya maamuzi ya kumkomoa bali anamuomba Mwenyezi Mungu atimize majukumu yake kwa busara,hekima na maarifa na kufufuata kanuni zilizopo.
Aidha Mh. Ngwada amewataka watumishi kufanya kazi na madiwani wote kama timu ili kuleta ustawi bora katika Halimashauri ya Manispaa ya Iringa.
Akiongea mara baada ya madiwani kuapishwa,Mkuu wa Wilaya ya Iringa ndugu Richard Kasesela amewataka madiwani kuhakikisha wanafunzi wote walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Manispaa wanapata nafasi na kuanza masomo ifikapo Januari 2020.
Kasesela pia amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ndugu Hamid Njovu kwa ujenzi wa shule mpya za sekondari ikiwemo ya Isakalilo na shule ya sekondari Igumbilo,kwani zitapunguza changamoto ya upungufu uliopo wa madarasa kwa shule za sekondari.
Mkurugenzi wa Maniapaa ya Iringa na katibu wa baraza la madiwani Hamid Njovu amewapongeza madiwani wote kwa ushindi walioupata na kuomba waridhie umaliliziaji wa miradi iliyopoya maendeleo katika kipindi cha miezi sita,ndipo waanze kutekeleza miradi mipya,ombi ambalo lilipokelewa kwa mikono miwili na mh.Meya pamoja na madiwani wote.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa