Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe.Ibrahim Ngwada leo Mei 19. 2023 ameongoza Baraza la Madiwani na Mwenyekiti wa Ccm Milaya ndugu Said Lubeya katika ziara ya kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Rungwe
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Kiwanda cha Maziwa ASAS kilichopo eneo la Ilenge ambapo Madiwani wamejionea namna kilivyoinua Sekta ya ufugaji katika wilaya ya Rungwe,kiwanda hicho kimefanya uwekezaji wa sh bilioni 3 na kinakusanya lita 20,000 za maziwa kwa siku ambapo kimeajiri vijana wapatao 42 ambao wanakusanya maziwa kutoka vijijini kuyaleta kiwandani hapo.
Kwa sasa kiwanda kinakusanya maziwa lakini ifilapo Juni mwaka huu kitaanza kusindika maziwa katika eneo hilo la ILENGE
Mradi mwingine ni jengo la kuhifadhia mali mbichi (cold room) lililopo katika Ukanda wa uwekezaji Ilenge Kata ya Kyimo ambapo wallpata fursa ya kujifunza namna mazao ya Parachichi yanavyo safirishwa na kuhifadhiwa katika jengo hilo linalomilikiwa na Halmashauri.
Pia Madiwani wamejionea jinsi Halmashauri inavyovutia wawekezaji kwa kutenga ardhi na kuweka miundombinu wezeshi ya uwekezaji kama maji, umeme, barabara na majengo.
Awali akiwakaribisha Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe.Mpokigwa Mwankuga amesema Wilaya ya Rungwe imebarikiwa ardhi nzuri kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwepo ufugaji, kilimo na vivutio vingi vya utalii na kuwakaribisha Madiwani wa Manispaa ya Iringa kuwekeza wilayani humo.
Ibrahim Ngwada ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa ameshukuru uongozi wa Wilaya ya Rungwe kwa ukarimu na kusema kuwa amejifunza mambo mengi mazuri na kuvutiwa na namna umoja wa wanawake wafugaji Rungwe (UWAWARU) wanavyofanya shughuli zake na kuahidi kuyafanyia Kazi pindi atakqporudi Manispaa kwa lengo la kuleta maendeleo Katika Halmashauri, huku Mwenyekiti wa CCM Wilaya ndugu Said Lubeya akiwapongeza kampuni ya ASAS DIARIES Kwa uwekezaji mkubwa wanaoufanya Manispaa ya Iringa pamoja na Wilaya ya Rungwe.
Lubeya amesema ipo haja Halmasuri ikaongeza idadi ya wafugaji wa Ng"ombe kwani kuna uhakika wa soko la maziwa,Pia amewapongeza wilaya ya Rungwe kwa jitihada wanazofanya kuhakikisha wanafanya vizuri katika Sekta ya ufugaji wilayani hapo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa