Mkiwa mnawasilisha hoja na mawazo yenu katika baraza mkumbuke kuwa mnawasilisha mawazo ya wananchi, hivyo fursa ya kuwepo hapa iwasilishe utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa maslahi ya nchi yetu na wananchi wetu.”
Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Alex Kimbe baada ya kuapishwa kwa madiwani sita ambapo madiwani watano wametoka kwenye kata za Ruaha, Gangilonga,Mkwawa,Mwangata na Kwakilosa na diwani mmoja wa viti maalum.
Amesema Kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 Manispaa ya Iringa imekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 83 hivyo ni vema madiwani wakashirikiana na wataalamu katika kubuni vianzia vipya na jinsi ya kukusanya mapato kuliko kuja kwenye baraza na maslahi ya mtu binafsi.
Naye mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela amesema kuwa wamachinga waliopo barabarani wasiondolewe mpaka hapo Manispaa itakapo tenga maeneo rafiki kwao kufanya biashara zao, kama ambavyo Rais ameagiza.
Kauli hiyo ya Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya imekuja baada ya mkurugenzi kuulizwa swali la papo kwa papo kuhusu wafanya biashara wadogowadogo kuziba baadhi ya barabara na kusababisha msongamano wa magari na ajali.
Amesema wataalamu wawajibike kwenye nafasi zao katika kuwahudumia wananchi na kwa kufanya hivyo wananchi wataipenda serikali yao.
Aidha madiwani sita wamekula kiapo cha kutunza siri na kupewa vitendea kazi, ili kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa