Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wametakiwa kufanya kazi kwa uadilfu na umakini mkubwa kwani jamii inamatarajio makubwa sana kutoka kwao.
Hayo yamesrmwa leo tarehe 15/12/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa na ndugu Ditram Mhoma Mkuu wa dawati la Elimu kwa umma Mkoa wa Iringa kwenye maelekezo na mafunzo kwa waheshimiwa madiwani.
Ndugu Mhoma amewataka waheshimiwa Madiwani wajiepushe na vitendo vya rushwa katika utendaji wao wa kazi kwani vitendo hivyo havitavumilika na wakifanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria jambo ambalo sio jema kutokea katika jamii.
Katika Mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halimashauri ya Manispaa ya Iringa ndugu Hamid Njovu amewataka Madiwani kuungana na wataalamu kutatua changamoto zilizopo kama upungufu wa zahanati na vituo vya Afya katika kata 18,,kutatua changamoto ya upungufu wa madarasa katika shule za sekondari zilizopo Manispaa
Aidha Njovu amewataka waheshimiwa Madiwani kujali muda wa vikao vya Halmashauri na kuzingatia kanuni,sheria na taratibu zilizopo kwa kuvaa mavazi nadhifu.
Akifunga kikao hicho Mh.Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwada amewaomba wataalamu kuwathamini na kuwapa hadhi inayostahili Madiwani wote, kwani kwa kufanya hivyo Halmashauri itafanya kazi na waheshimiwa Madiwani kwa ushirikiano na umoja na kuwaletea wananchi maendeleo katika kipindi kifupi.
Katika kikao hicho taasisi mbalimbali zilipata fursa ya kutoa mada taasisi hizo ni, Nmb Bank,Crdb Bank,Bima,na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa