Uongozi wa Mkoa wa Iringa umetakiwa kuhakikisha unatekeleza miradi mbalimbali inayotokana na fedha za Uviko 19 zilizotolewa na Serikali kupitia mkopo uliotolewa na shirika la fedha Duniani (IMF)
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa(MNEC) Mkoa wa Iringa Salim Abri katika mkutano wa Madiwani wote wa Mkoa wa Iringa uliofanyika ukumbi wa Royal Palm ,ukiwa na lengo la kuwakutanisha madiwani hao na viongozi wa juu wa Serikali.
"Utekelezaji wa miradi hii ni muhimu kuzingatia viwango katika kupunguza changamoto zilizotokana na Uviko 19, janga lililo tikisa dunia ikiwemo Tanzania." Alisema Abri.
Katika hatua nyingine Abri amewakumbusha Madiwani hao kuwa fedha hizo ni za mkopo na sio msaada.
"Fedha hizi ni mkopo na Serikali itatakiwa kurejesha fedha hizi japo kuwa siyo kwa riba."
Sanjari na hayo Akizungumzia mkutano huo kuwa lengo lake kuu ni kuzungumzia agenda ya utekelezaji wa Ilani CCM.
Huku akiwa pongeza Madiwani hao kwa kuandaa mkutano huo ambao utafanya mabadilishano ya maendeleo kati ya Halmashauri na halmashauri ,kata na kata ili kuendelea kuleta maendeleo nakutekeleza ilani ya chama hicho.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada,ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi katika Halmashauri ya Manispaa ambazo zimefanya kazi nyingi katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwepo umaliziaji wa machinjio ya kisasa yaliopo Ngelewala ambayo likuwa tatizo kubwa katika Halmashauri .
Pia umaliziaji wa wodi ya hospitali ya Frelimo,umaliziaji wa madarasa 33 katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa pamoja na umaliziaji wa maboma ya madarasa katika maeneo ya Halmashauri .
"Katika mapato yetu ya Halmashauri tumeweza kuhakikisha tunatekeleza miradi mbali mbali mkienda katika jengo letu la stendi ya Igumbilo tunamalizia, pia tunayo madarasa tunamalizia na maeneo mengine mengi na tunatekeleza kupitia makusanyo yetu, kupitia mapato yetu ya ndani pia tumetoa asilimia 10% kwa akina wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ,kwakweli tumehakikisha pesa hizo zinakwenda kwa wahusika,"alisema Gwada
Mkutano huo pia umehudhuriwa na Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Iringa Bi. Happiness Seneda ambaye pia amepata nafasi yakutoa takwimu juu ya lishe,vita dhidi ya ukimwi ,mpango mkakati kuhusiana na mazingira ,miradi ya maendeleo na bajeti pamoja na suala la unyanyasaji wa kijinsia kwa akina mama ,watoto na akina baba.
Hivi karibuni Serikali ya Tanzania imepokea Shilingi trioni 1.3 za kukabiliana na athari za janga la UVIKO-19 kutoka IMF na kugawa kwenye kila Mkoa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa