• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Environment and Cleaning
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Kazi
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma ya elimu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba

MADIWANI/WATAALAM MANISPAA YA IRINGA WAPEWA ELIMU JUU YA VVU UKIMWI

Posted on: July 10th, 2021

Iringa Manispaa ni miongoni mwa Wilaya 65 Tanzania  zinazotekeleza mradi wa HEBU TUYAJENGE chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani( USAID) chini ya usimamizi wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na maambukizi ya VVU UKIMWI

Shirika la Centre for women and children development(CWCD limeendesha mafunzo hayo kwa timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhusu gurudumu la rufaa(Bi-directional referrals and linkeges) kwa lengo la kuongeza uelewa kwa waheshimiwa Madiwani kutoka kata 5  za mradi ambazo ni Kihesa,Mkwawa,Igumbilo, Isakalilo na Ruaha. Katika kutekeleza mradi huo Madiwani pamoja na wataalam wamepewa mafunzo ya namna ya kuibua vijana na watoto wenye viashiria vya VVU UKIMWI ili waweze kupimwa afya zao na kuanza kutumia dawa

Akitoa mada katika mafunzo hayo  Bi.Happy Josephat amesema iko tamko la Serikali kuhusu ridhaa ya vijana wenye umri wa miaka 15 linaelekeza kuwa kijana mwenyewe anayo ridhaa ya kupima VVU UKIMWI bila ridhaa ya mzazi hivyo amewataka wajumbe kutoa elimu hiyo katika jamii

Ameeleza kuwa changamoto kubwa kwa vijana kutojitokeza kupima VVU UKIMWI ni ukosefu wa huduma rafiki kwa vijana  kwenye vituo vya afya  hivyo kupelekea vijana kushindwa kujitokeza kupata huduma

Aidha amesema malengo ya kimkakati ni kuhakikisha wanafikia asilimia95 watu kupima VVU UKIMWI 95 waliopima wenye maambukizi  waanze dawa 95 Wabaki kwenye dawa ili kufubaza VVU kwenye damu  

Bi.Josephat amesema mpango kazi waliojiwekea kwenye mafunzo hayo ni Halmashauri kuhakikisha  inaibua vijana na watoto,pia wenye maambukizi ya VVU kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika vikao vyote vya Kata na Mitaa  ili waweze kutoa elimu

Kwa upande wake Naibu Meya mhe.Kenyata likotiko amelishukuru Shirika la CWCD kwa kutoa mafunzo hayo kwanikwa watu sahihi na kuwa wao ndiyo viongozi wa wananchi itakuwa rahisi kuwafikishia elimu waliyoipata na kuleta matokeo tarajiwa

Mheshimiwa Eliud Mvela ni Mwenyekiti wa huduma za jamii anasema kazi kubwa waliyonayo ni kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya Madiwani wataalam,viongozi wa Konga ili kuifikia jamii  kwakufanya ufatiliaji wa karibu ili kutimiza mpango mkakati waliojiwekea

Kaimu Mkurugenzi Dr.Jesca Lebba amesema atahakikisha mikakati yote iliyowekwa inatekelezwa kwa wakati na kuahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi wa konga pindi watakapopata changamoto za kitaalam wakati wanatekeleza majukumu yao

Mafunzo hayo yamefadhiliwa na USAID,PEPFAR,CWCD na NACOPHA yamefungwa leo tarehe 10/7/2021 na Katibu Tawala Wilaya ndugu Eston Kyando ambaye amewataka  washiriki kuyatendea kazi ili yaweze kuleta matokeo chanya.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUCHUKUA FOMU YA UJENZI WA JENGO LA BIASHARA TEMBO BAR February 15, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA, 2023/2024 July 13, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI July 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 23, 2024
  • Soma zote

Habari za Hivi punde

  • PPP CENTRE YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU IRINGA MC

    April 04, 2025
  • ALUTE: "HAKIKISHENI MIRADI INAKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA UBORA"

    December 21, 2024
  • UCHAGUZI HURU NA WA HAKI UNAHITAJI USHIRIKISHAJI - RC SERUKAMBA

    October 10, 2024
  • MSIGALA AWAONYA MAAFISA MAENDELEO KUJIHUSISHA NA MIKOPO HEWA

    October 05, 2024
  • Soma zote

Video

MEYA WA MANISPAA KUZIPIGANIA TIMU ZA MKOA KUPANDA DARAJA
More Videos

Viunganisho vya Haraka

  • National Examination Council of Tanzania
  • Watumishi Portal
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA,2023/2024
  • Sheria ndogo za Manispaa
  • Vivutio vya Utalii na Taarifda zake
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tovuti Zinazofanana

  • Goverment Website
  • TAMISEMI
  • Iringa Region Website
  • IMtv Fahari ya Iringa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

Location Map

Wasiliana nasi

    Iringa Municipal Council

    Sanduku la Posta: 162

    Telephone: +255-2702647

    Mobile: 255-2702647

    Email: md@iringamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya usiri
    • Ukanusho
    • MMM
    • Ramani ya eneo
    • Huduma zetu

hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa