Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imetenga kiasi cha shilingi milion 40 kwa ajili ya umaliziaji wa bweni na madarasa katika Shule ya Watoto wenye Mahitaji maalum Ipogolo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndg. Kastory Msigala mbele ya Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Mobhare Matinyi na waandishi wa habari wakati akieleza Maendeleo yaliyofanyika ndani ya Manispaa ya Iringa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan.
Akijibu swali lililoulizwa na Miongoni mwa Waandishi wa habari juu ya kutomalika kwa majengo mawili yaliyojengwa kwa muda mrefu moja jengo lenye vyumba vya madarasa mawili pamoja na bweni katika shule hiyo ya Watoto wenye Mahitaji maalum Ipogolo amesema halmashauri inatambua juu ya changamoto hii na tayari fedha imetengwa kiasi cha sh milion 40 kwa ajili ya umaliziaji ili majengo hayo yaanze kutumika.
"...ni kweli ndugu mwandishi majengo hayo yamejengwa ni kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na kwa kutambua umuhimu wa suala hilo tayari halmashauri imetenga fedha kiasi cha shilingi milion 40 ambayo hii itasaidia juu umaliziwaji wa majengo hayo yaanze kutumika kwa ajili ya wanafunzi wetu...." Msigala
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa