Ujenzi wa Majengo ya Kitega Uchumi katika eneo la stendi ya zamani ya mabasi (Tembo Bar) pamoja na Jengo la Ghorofa mbili la Community Centre eneo la Kitanzini yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa baada ya kukamilika.
Hayo yamebainishwa katika ziara ya Kamati ya Fedha na Uongozi kwa kipindi cha Robo ya Tatu Januari - Machi 2023/2024 walipotembelea na kukagua miradi hiyo na kuona mafanikio na changamoto zilizopo.
Afisa Uwekezaji Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Amiry Mtamike amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa Mradi wa ujenzi wa Jumba la Maendeleo (Comunity Centre) ambao utagharimu zaidi ya Tsh Bilioni 1.8 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri na Magereza kwa kipindi cha miezi 12 ambapo ulianza kutekelelezwa, mwezi Januari mwaka 2023 ambapo katika jengo hilo chini kutakuwa na Maduka 28, ATM, Min-Supermarket na Duka la Dawa, huku ghorofa ya kwanza kutakuwa na ukumbi mkubwa wa mikutano na ghorofa ya pili kutakuwa na kumbi ndogo 4 za mikutano.
Mtamike amesena kuwa mradi wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi Tembo Bar utagharimu zaidi ya Tsh Bilioni 2.6, mradi huu utatekelezwa kwa mfumo wa jenga, endesha, kabidhi ambapo wafanyabiashara watashirikiana na Halmashauri kutekeleza mradi huu kwa makubaliano maalumu ambayo yatasimamiwa na Mwanasheria wa Manispaa ya Iringa katika kuingia makubaliano hayo.
Mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada ameitaka Menejimenti kuongeza juhudi ya usimamizi wa ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati na kuleta manufaa kwa wananchi na Halmashauri kwa ujumla.
“Nataka kuona ujenzi unaendelea kwa kasi na vifaa vyote vinavyohitajika vinafika eneo la kazi kwa wakati hali hii hairidhishi hivyo ongezeni kasi ili ujenzi ukamilike kwa wakati.” Amesema Mhe. Ngwada.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Kastori Msigala amesema amepokea maelezo yote ya Kamati na kuahidi kuyafanyia kazi kwa wakati.
Ujenzi huu utafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa vyumba 100 vya maduka ghorofa ya kwanza na awamu ya pili itakuwa ni ujenzi wa vyumba 60 vya kulala katika ghorofa ya pili.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa