Maonesho ya Kimataifa ya UTALII KARIBU KUSINI yamehitimishwa leo tarehe 13/11/2022 katika eneo la Kihesa Kilolo Manispaa ya Iringa .
Akifunga maonesho hayo Mgeni rasmi Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Othman Othman amewata wakuu wa Mikoa kumi ya Nyanda za juu Kusini kuendelea kuyatangaza maonesho hayo ili yaweze kuwavutia wananchi wengi zaidi wa Mikoa hiyo na mikoa ya jirani pamoja na wageni kutoka nje ya nchi.
Mhe .Othman amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege Nduli na Songwe ili kuwafikisha watalii wengi zaidi katika vivutio vilivyopo nyanda za juu kusini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego amewapongeza wadau na waandaaji wa maonesho hayo ambapo ameeleza kuwa maonesho hayo yametoa fursa mbalimbali kwa wakazi na wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa na Mikoa ya karibu kuonesha na kuuza bidhaa mbalimbali za utalii na kunufaika na maonesho hayo.
Maonesho hayo ya wiki nzima yamefanyika Mkoani Iringa kwa mara ya tatu na kuhudhuriwa na wananchi, viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali,wafanyabiashara ,Taasisi na makampuni ambapo walipata fursa ya kuonesha na kuuza bidhaa za utalii.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa