Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Bi, Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi ngazi ya Mkoa na mashirika yaliyo katika Mkoa wa Iringa kufanya ziara za mara kwa mara kwa wananchi kwani wananchi wanahitaji elimu sana huko chini lakini hawafikiwi na viongozi hao.
Makamu wa Rais ameyasema hayo alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake Mkoani Iringa ziara iliyodumu kwa siku 4 ambapo alifanya ziara katika Wilaya za Mkoa wa Iringa.
Amesema wingi wa watu aliouona kwenye mikutano yake ya hadhara unaonyesha dhahiri kuwa wananchi wanakiu ya kuwaona viongozi wao au wanahitaji sana elimu kutoka kwa viongozi. Ameongeza kuwa wakuu wa mashirika pia wawatembelee wananchi na kuwapa elimu kuhusu shughuli zinazotolewa na mashirika yao. Kwa kufanya hivyo watakuwa wametibu kiu ya wananchi.
Katika Manispaa ya Iringa Makamu wa Rais ametembelea kiwanda cha Ivory na kiwanda cha uzalishaji wa mbogamboga kilichopo Kibwabwa na baadae kupata taarifa ya Mkoa.
Aidha siku ya jumatatu tarehe 12/2/2018 Makamu wa Rais alipata fursa ya kufanya mkutano wa hadhara na wananchi katika eneo la Mwembetogwa katika Manispaa ya Iringa.
Makamu wa Rais pia amezindua Mradi wa Uendelezaji wa Maliasili na Utalii kusini mwa Tanzania yaani (REGROW) katika eneo la Kihesa Kilolo ambapo Mradi huo umefadhiriwa na Benki ya Dunia na utasaidia kukuza utalii kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini.
Kuhusu suala la wamachinga Makamu wa Rais ameutaka uongozi wa Manispaa kurasimisha shughuli za wamachinga ili watambulike na kusaidiwa wakiwa kwenye makundi pia amewataka wawe na vitambulisho vitakavyo wasaidia kutambulika kwenye umoja wao bila kusahau kujiunga na mifuko ya afya na taasisi za kifedha.
Mwisho amewapongeza Manispaa ya Iringa kwa juhudi walizofanya kimaendeleo katika sekta mbalimbali na kuahidi kuwasaidia kwa baadhi ya changamoto katika shughuli zao za maendeleo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa