Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Paul Christian Makonda amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Kastori Msigala kushughulikia madai ya malipo ya mstaafu, ndg.Michael Chadewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembettogwa tarehe 8 Februari 2024 Mjini Iringa .
Akisikiliza kero mbalimbali za wananchi kwenye mkutano huo ambapo mstaafu huyo amesema kuwa alikuwa mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa (Mwaka 1966- 2005).
Chadewa amesema pamoja na kufuatilia madai yake kwa muda nrefu mpaka sasa bado hajalipwa,hivyo anaoomba ndg Makonda kumsaidia ili apate haki yake.
"Baada ya kustaafu Mwaka 2005, nilikwenda PSSF kufuatilia mafao yangu nikaambiwa jina langu halipo na kwenda kwa Mkurugenzi ambaye alikuwa mwajiri wangu. akaniambia hayo ni makosa ya ofisi ndio maana jina lako halipo, akasema atashughulikia", amesema mzee Chadewa.
Mheshimiwa Makonda aliutaka uongozi wa Halmashauri kuthibitisha madai ya mzee huyo na kumlipa mara moja.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe. Ibrahim Ngwada amekiri"kufahamu suala hilo na kwani Mzee Chadewa alifika ofisini kwake amesema madai ya Ndg.Chadewa ni ya kweli nilishaanza kushughulikia na nyaraka zake zilithibitishwa Mkoani na kuonekana ni za kweki hivyo nikiri kuwa kubadilika kwa uongozi Manispaa(wakurugenzi) kulichelewesha upatikanaji wa haki yake hivyo nimuombe mzee Chadewa Ijumaa tarehe 9.2.2024 afike ofisini tushughulikie taratibu za malipo yake amesema Ngwada.
Wakati huo huo ndg. Makonda alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ndg Kastori Msigala kumpatia mzee huyo kiasi cha shilingi laki nne kama kifuta jasho kwa ufuatiliaji wa muda mrefu wa madai yake Mkurugenzi alitekeleza agizo hilo kwa kumpatia fedha taslim shilingi lali nne( 4)
Huo ni muendelezo wa ziara za Mheshimiwa Makonda ambazo zinafanyika mikoa 20 Tanzania bara kwa njia ya mikutano ya hadhara lengo likiwa ni kusikiliza kero mbali mbali za wananchi na kuzitatua papo hapo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa