Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya darasa la saba ya kuhitimu elimu ya msingi 2021 ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imekuwa miongoni mwa halmashauri 10 bora zilizofanya vizuri kwa kushika nafasi ya sita kitaifa.
Aidha, Mkoa wa Iringa umeshika nafasi ya pili kitaifa katika matokeo hayo ikitanguliwa na kinara Mkoa wa Dar es Salaam, nafasi ya tatu ikienda kwa Mkoa wa Mbeya, nne Mkoa wa Arusha na nafasi ya tano ikienda kwa Njombe.
Akitangaza matokeo hayo Jumamosi Oktoba 30, 2021, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alizitaja halmashauri zilizoingia kumi bora kitaifa kuwa ni Halmashauri ya Jiji la Ilala, Halmaahauri Jiji la Arusha, Halmashauri Maniapaa ya Kinondoni, Halmaahauri ya Manispaa ya Moshi, Halmaahauri jiji la Mwanza, Halmashauri Manispaa ya Iringa.
Nafasi ya saba imeshikiliwa na Halmashauri Manispaa ya Ilemela ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji Mafinga, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na nafasi ya kumi imekwenda kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Dk.Msonde alisema katika mtihani huo watahiniwa waliofanya mtihani huo 907,802 wamefaulu na kubainisha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.89.
“Watahiniwa 907,802 kati ya 1,107,460 waliotunukiwa matokeo wamefaulu. Watahiniwa hawa wamepata alama 121 au zaidi kati ya alama 300” amesema.
Amesema kati ya hao wasichana ni 467,967 (asilimia 81.43) na wavulana ni 439,835 (82.56).
“Mwaka 2020 idadi ya watahiniwa waliofaulu ilikuwa 833,672 hivyo idadi ya watahiniwa waliofaulu mwaka 2021 imeongezeka kwa watahiniwa 74,130 sawa na asilimia 8.89 ukilinganisha mwaka 2020” amesema.
Mwisho
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa