HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa, imejipanga kutekeleza agizo la Serikali la kuwapanga na kuwajengea vibanda vya kufanyia biashara zao wafanyabiashara wadogo maarufu Wamachinga katika maeneo mapya manne ambayo yamependekezwa ikiwa ni mkakati wa kukuza na kuinua mji kiuchumi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Mhe.Ibrahim Ngwanda, alitangaza mkakati huo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mshindo kwenye mkutano wa hadhara ambao alitumia fursa hiyo kuwaeleza mikakati mbalimbali iliyowekwa na halmashauri katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mhe.Ngwanda alisema maeneo yaliyopendekezwa ambayo wamachinga watapangiwa ni eneo la Maghorofani Kitanzini ambapo vitajengwa vibanda 350 na eneo la Gereji bubu.
Maeneo mengine watakakopangiwa wamachinga ni eneo la Soko la Mlandege ambapo vitajengwa vibanda kwenye uzio wa makaburi na eneo la ofisi ya kata ya Mshindo.
Mhe.Ngwanda alisema matumaini ya Manispaa ni kwamba wamachinga wakihamishiwa maeneo hayo kutasaidia kukuza na kuinua mji kiuchumi.
Mstahiki Meya akizungumzia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata ya Mshindo, alisema Manispaa imejipanga kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara tatu katika kipindi cha miaka miwili mitatu ijayo kwa kuanzia mwaka huu wa fedha.
Mhe.Ngwanda alizitaja barabara ambazo zipo katika mpango wa kujengwa kuwa ni barabara ya Mshindo na Mtwa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa