Timu ya Sekretarieti ya Mkoa wa Iringa imefanya ziara ya ukaguzi wa baadhi ya miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa ya Iringa na kuwataka waongeze kasi ya ujenzi kwani mwisho wa utekelezaji wa miradi hiyo ni June 2021.
Akiongea wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo Afisa Tawala msaidizi Serikali za Mitaa ndugu Wilfred Myuyu amesema Halmashauri inatakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi,ikiwa ni pamoja na kufuata maelekezo ya ramani zilizoandaliwa kwa kufanya hivyo watakuwa wametekeleza wajibu wao ipasavyo na kufanya miradi hiyo ilete matokeo chanya kama ilivyokusudiwa.
Aidha Myuyu amesema maelekezo yote waliyoyatoa kwa ajili ya marekebisho kwenye miradi waliyopita yafanyiwe kazi haraka ili miradi hiyo ikamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Myuyu amewataka wataalam kusimamia kazi za ujenzi huo usiku na mchana kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliopangwa ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha Kamati imeupongeza uongozi wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa mradi wa Ujenzi wa Wodi ya wanawake,Wanaume,jengo la upasuaji pamoja na jengo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya wilaya Flerimo na kusema mradi huo wa mfano wa kuigwa.
Mradi huo ambao unatekelezwa baada ya kupokea kiasi cha shilingi milioni mia saba Tsh 700 000,000/= kutoka Serikali kuu na ukikamilika utatoa huduma kwa wanachi wa Manispaa ya Iringa na Mkoa kwa ujumla.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndugu Charles Mwakalila amesrma amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na sekretarieti na kuahidi kuyafanyika kazi mara moja ili kuwaletea maemdeleo wananchi wa Manispaa
Miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa Kituo cha Afya Mkimbizi,kituo cha Afya Itamba na Machinjio ya kisasa Ngelewala.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa