Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imepokea Hundi ya kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano kutoka katika Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa thelathini na mbili (32) unaoendelea katika baadhi ya shule za Sekondari Manispaa ya Iringa.
Akipokea mchango huo Mwenyekiti wa harambee ya Ujenzi wa Madarasa Bw. Kasimu Majaliwa ambaye ni Afisa Biashara wa Manispaa amewashukuru Shirika la Bima la Taifa kwa mchango ambao wametoa na kuahidi kutekeleza kujenga madarasa hayo kwa kiwango bora.
Shirika la Bima la Taifa limeahidi kuendelea kuwa bega kwa bega katika kuendeleza kuchangia maendeleo hasa katika upande wa elimu.
.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa