Baraza maalumu la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa limepitisha makadilio ya Bajeti ya mwaka wa Fedha 2018/0219 ya shilingi 45 billioni huku kipaumbele kikiwa ni kuboresha miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Akiwasilisha makadilio ya Bajeti ya mwaka 2018/2019 mbele ya Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, Mchumi wa Manispaa Msifwaki Haule amefaafanua kuwa kiasi cha shilingi 29 bilioni kitatumika kulipa mishahara, 3 bilioni ni matumizi ya kawaida na 12.5 bilioni ni matumizi kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Baraza hilo la kupitisha makadilio ya Bajeti kwa Halmashauri ya Manipspaa ya Iringa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, wajumbe wa baraza la madiwani pamoja na wataalamu
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa