Manispaa ya Iringa imeahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kutoka katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwaaajili ya kusaidia kikundi cha wanawake cha Jordan kinachojishughulisha na ufugaji wa kuku kutoka kata ya Mkimbizi chenye wanachama 11 chini ya Kamati ya kudhibiti Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa na Meya wa Manispaa ya Iringa kama Msimamizi wa Halmashauri kwa kikundi hicho baada ya kamati ya Kudhibiti Ukimwi inayoongozwa na Diwani wa Kata ya Mshindo mheshimiwa Ibrahimu Ngwada Kutembelea kikundi hicho.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Ngwada, amesema anaomba ahadi hiyo ya Halmashauri itekelezwe mara moja kwani kikundi hicho ni moja ya kikundi kilichoamua kusimama na kuunda umoja wa wanawake wanaoishi na maabukizi ya ukimwi wakiwa na lengo la kujikwamua kiuchumi na kufuatilia matumiazi ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi.
Amesema inatia moyo kwa kuona wanawake hao wamejikubali na kushauri vikundi kama hivi viundwe katika Kata zote.
Akisoma taarifa kwa Kamati hiyo, Katibu wa Kikundi hicho amesema kwa sasa kikundi kina jumla ya kuku wapatao 180 wa mayai ambapo kwa siku moja wanaokota tray tatu za mayai na kuziuza kwa shilingi elf saba kwa tray moja.
Adha kikundi cha Jordan kimeweza kujiinua kiuchumi kwa kununua hisa kwa kila mwanachama na kukopeshana.
Kamati pia imeweza kutembelea hospitali ya frelimo inayomilikiwa na Manispaa ya Iringa na kujiona jinsi ambavyo huduma ya tohara inafanyika na kujua changamoto ya utoaji wa uhudu hiyo.
Akitoa taarifa kuhusu huduma ya tohara hospitalini hapo Mganga mfawidhi wa hospitali ya Frelimo Drk. Pilila Zambi amesema mpaka sasa wanaume wapatao 1996 na watoto 979 wameshafanyiwa tohara katika kituo hicho.
Amesema tohara inapunguza maambukizi ya ukimwi kwa asilimia 60 hivyo ni vyema wanachi ambao hawajapata huduma ya tohara wakahamasishwa kufanya hivyo.
Amesema changamoto kubwa wanayoipata kituoni hapo ni muitikio mdogo wa wazazi ambao wanashindwa kuwaleta watoto wadogo kupata huduma ya tohara wakiamini kuwa tohara katika umri mdogo hufanya maumbili ya motto kushindwa kukua jambo ambapo sio la kweli.
Hivyo mwenyekiti wa Kamati na wajumbe kushauri elimu kuzidi kutolewa kwa wazazi, kwenye vyombo vya habari na mikutano ya kijamii ili wanachi waweze kufahamu umuhimu wa toharakwa watoto wa kiume.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa