Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango amekabidhi cheti pamoja na zawadi ya fedha Tsh. Milioni moja kwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada mara baada ya Halmashauri hiyo kuibuka mshindi wa 3 kati ya Manispaa 184 katika mashindano ya Afya na Mazingira kundi la Halmashauri za Manispaa Tanzania Bara mwaka 2024.
Zawadi hiyo ilikabidhiwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa niaba ya mgeni rasmi katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Kampeni ya “Mtu ni Afya” awamu ya pili yenye kauli mbiu inayosema “Mtu ni Afya,Afya Yangu Wajibu Wangu” , uliofanyika eneo la Stendi ya zamani Maili moja Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Mei 09 2024.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Naibu waziri wa TAMISEMI Mhe. Festo Dugange, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Alhaj. Abubakar Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba na Katibu Tawala Wilaya ya Iringa ndg. Michael Semindu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Komrade Daud Yassin, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada, Naibu Meya wa Manispaa Iringa Mhe. Julius Sawani, Mwenyekii wa Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu Mhe.Eliud Mvella, Kaimu Mkurugenzi Manispaa Dkt. Godfrey Mbangali, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya-Pwani, Wataalamu wa Afya kutoka Manispaa ya Iringa, Wanachi, na Wasanii mbalimbali.
Akizungumza katika hafla hiyo Dkt Mpango amesema ili kufanikisha kampeni hii atatumia wadau mbalimbali huku akiwataja wasanii pamoja na wanahabari kuwa na nafasi kubwa ya kuhamasisha na kuujulisha umma na kufikisha ujumbe kama ambavyo tayari wamekwisha kuanza kufanya kupitia awamu ya kwanza na huku akizitaka Halmashauri kuwatumia vizuri wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika kutoa elimu zaidi katika masuala ya afya na usafi.
“Watumieni vizuri wahudumu wa afya ngazi ya msingi kwani kwa kufanya kampeni na itakuwa na mafanikio makubwa, viongozi wa Serikali za Mitaa wekezeni katika kudhibiti taka ngumu, maji taka ongezeni kasi ya ujenzi wa Mitaro, utoaji taka kwa wakati na zijengeeni uwezo timu za Menejimenti kwa kufanya hivyo mtaepusha magonjwa ya mlipuko katika maeneo yenu. Amesema Dkt.Mpango
Mstahiki Meya Mhe. Ibrahim Ngwada amesema siri ya mafanikio hayo ni uwekaji wa mapipa ya taka (dustbin) katika maeneo yote ya Halmashauri ikiwa ni pamoja na maeneo ya pembezoni mwa barabara, kuwa na utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara na kulinda afya ya jamii kwa watalaamu kutoa elimu ya kujikinga na mgonjwa ya mlipuko pia ameahidi kufafanyia kazi maelezo yaliyotolewa na Mgeni rasmi Dkt. Mpango.
Mashindano haya hufanyika kila mwaka na kwa takribani miaka 5 mfululizo Manispaa imekuwa ikishika nafasi ya kwanza na ya pili kwa mwaka 2023 imeshika nafasi ya 3 huku ushindi wa ujumla wa usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora mwaka 2024, huku nafasi ya mshindi ya kwanza ikishikiliwa na Manispaa ya Shinyanga na nafasi ya pili ni Manispaa ya Moshi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa