Katika kuadhimisha siku ya Maziwa Duniani, Manispaa ya Iringa kwa kushirikiana na Kampuni ya maziwa ya ASAS imegawa maziwa kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Ipogolo pamoja na Shule ya Viziwi Mtwivila ikiwa ni sehemu ya uadhimishaji wa siku hiyo
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Lishe Manispaa ya Iringa Bi. Anzael Msigwa amesema maziwa ni sehemu muhimu sana ya lishe hasa kwa wanafunzi kwani huboresha afya zao na kupelekea ufaulu mzuri darasani.
‘’siku ya leo ni siku muhimu sana, ndiyo maana Manispaa inatekeleza hili kwa vitendo kwa sababu faida yake ni kubwa kama vile kuongeza uwezo wa kuona kwa wanafunzi wetu, kuzuia utoro na mengine mengi, kwa kipekee niwapongeze wadau wetu kampuni ya Asas kwa kuwezesha siku hii kwenda kama ilivyopangwa’’
Kwa upande wake Mwl. Mkuu shule ya msingi Ipogolo Isaya Sekwau ameipongeza Manispaa ya Iringa kwa kuichagua shule ya msingi ipogolo kama sehemu ya uazimishaiji wa siku ya maziwa duniani ambapo wanafunzi wa shule hiyo wamepata furusa ya kunywa maziwa hayo.
Nae Mwl. Mkuu shule ya Viziwi Mtwivila Bw. Allinanuswe Mwankosye amesema’’tunashukru sana kwa hiki mlichotuletea kwa wanafunzi wetu, hii itaongeza molali kwao na kwetu kwa heshima hii kubwa mliotupatia’’
Pamoja na hayo wadau katika siku hiyo kampuni ya maziwa ya Asas kupitia kwa Mratibu wake Bwana Mtimila Lipita amesema kuwa kampuni yao itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha inatoa huduma ya maziwa katika shule mbalimbali huku kipaumbele ikiwa ni shule zenye uhitaji maalumu.
Zaidi ya wanafunzi 2800 pamoja na Walimu kutoka shule za Msingi Ipogolo na Shule ya msingi viziwi Mtwivila wamekunywa maziwa kutoka kampuni ya uzalishaji wa maziwa ya ASAS Dairies Limited iliyopo Mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya kilele cha maazimisho ya siku ya Unywaji wa Maziwa Duniani
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa