Kaimu mkurugenzi Manispaa ya Iringa Dr.Steven Ngwale amewataka wafanyabiara wa Soko la mashine tatu kuzingatia usafi katika maeneo wanayofanyia biashara ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko. Dr Ngwale ametoa maelekezo hayo leo siku ya Jumamosi ya usafi. Amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kutekeleza agizo la Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli la kila mwananchi kuhakikisha anafanya usafi wa mazingira katika maeneo yanayomzunguka ifikapo kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Naye Mganga mkuu wa Manispaa Dr.Jesca Lebba amewapongeza wafanyabiashara kwa kujitokeza kwa wingi kufanya usafi. Dr Lebba amewaasa wafanyabiashara kuhakikisha wanakuwa na utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara ili kuzuia magonjwa na hivyo kupunguza gharama za matibabu.
Katibu wa wafanyabiashara wa soko la mashine tatu Bw Joseph kilienyi ameomba Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kutatua changamoto mbalimbali walizonazo wafanyabiashara ikiwemo kuziba kwa mifereji ya maji taka iliyopo maeneo ya soko.
Zoezi la usafi wa mazingira limefanyika eneo la mashine tatu kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa tatu asubuhi ambapo wafanyakazi wa Manispaa pamoja na wafanyabiashara wameshiriki kikamilifu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa