Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada ameta mifuko 50 ya saruji katika Shule ya Msingi Chemchem kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa choo chenye matundu 28 shuleni hapo
Mh. Ngwada ameonyesha mfano na kuitaka jamii kuchangia maendeleo ya elimu katika Manispaa ya Iringa kupitia shughuli mbalimbali za jamii
Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 12/01/2021 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi matukufu ya Serikali ya Zanzibar
Naye Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mhe. Jesca Msambatavangu amechangia mabati katika ujenzi huo wa choo katika Shule hiyo na kuahidi kama watakamilisha ndani ya wiki mbili atawakabidhi bati hizo
Nae Rais wa Serikali ya Chuo kikuu cha RUCU akiwa ameongozana na na kundi la umoja wa vijana wa CCM seneti tawi la RUCU ametoa kiasi cha sh 50,000/= ziweze kusaidia ujenzi huo
Wengine walio changia ujenzi huo ni pamoja na Diwani wa kata ya Mkimbizi Eliud Mvela ambaye amechangia sh 30,000/= na kusema jukumu la kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora ni letu jamii
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ndugu Hamid Njovu amesema anashukuru kupata Mbunge ambaye anajitoa kusukuma maendeleo ya wananchi wake
Awali maadhimisho hayo yalianza Katika Stendi mpya ya Igumbolo ambapo wananchi na taasisi mbali mbali walijitokeza katika uzinduzi wa upandaji miti ambapo miti 500 ilipandwa katika eneo hilo
Waliojitokeza katika maadhimisho hayo ni vikundi mbalimbali vya usafi wa mazingira, wananchi, Envbright, MWAKIMC, Cleaners Health na umoja wa vijana CCM Seneti tawi la RUCU, Tawagro na Waheshimiwa madiwani wa chama cha Mapinduzi Manispaa
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa