Jana Juni 17.2021 Halmashauri ya Mansiapaa ya Iringa imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya kijinsia na watoto, iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nyumba tatu
Maadhimisho hayo yaliyobeba ujumbe wa 'TUTEKELEZE AJENDA 2040 : KWA AFRIKA INAYOLINDA HAKI ZA MTOTO' yamewakutanisha watoto na wanafunzi kutoka shule mbali mbali za msingi za Manispaa ya Iringa
Akizungumza katika maadhimisho hayo Ndg. Eston Kyando Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa qmbaye alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya kama Mgeni rasmi amekemea baadhi ya familia kuwabagua watoto kijinsia katika elimu na mahitaji mengine ya muhimu
"Serikali imelipia Elimu kwa kila mtoto hivyo wazazi tusiwaache watoto wakakosa kuelimika tuwapeleke wakasome kwa ajili ya taifa bora la Tanzania ya baadae" alisema Ndg. Kyando
Tiniel Mbaga ni Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa, ameeleza kuwa Ofisi yake inaendelea kutoa elimu kwa Jamii katika kukomesha ukatili wa kujinsia kwa watoto na ametoa wito kuanzia ngazi ya familia kuhakikisha wanawalinda watoto dhidi ya ukatili na amesema yeyote atakayebainika kumfanyia ukatili mtoto basi sheria kali zitachukuliwa dhidi yake
Afisa Maendeleo ya Jamii, Mwantumu Dosi amewashukuru wadau kujitokeza katika kushiriki kwenye maadhimisho hayo pia ameeleza kuanzishwa kwa mabaraza ya watoto kwa ngazi ya kata na Halmashauri huku akieleza kuwa hatua hiyo itawasaidia watoto hao kujadili changamoto zao ili ziweze kutatuliwa na ni dhana itakayowajengea kuwa viongozi wa badae
Ikumbukwe kuwa madhimisho ya mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka Juni 16 ambapo kwa Mkoa wa Iringa yalifanyika Kiponzelo huku mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa