Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kushirikiana na wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,inatarajia kuanza zoezi la ugawaji vyandarua ndani ya Manispaa katika kata zote kumi na nane.
Katika kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi watendaji wa kata 7, watendaji wa mitaa 7,maafisa Afya, pamoja na wanajamii wa kujitolea leo wamepewa mafunzo ili kuhakikisha kaya zote zilizopo katika Manispaa ya Iringa zinaainishwa,zinatambuliwa,idadi ya walengwa kwa lengo la kuwagawia vyandarua vyenye viatilifu wa muda mrefu.
Regina shigongo ni Afisa afya Manispaa ya Iringa akitoa mada katika mafunzo hayo amewataka washiriki kuzingatia mafunzo waliyopewa ili waweze kufanya kazi hiyo kwa weledi.
Nae mratibu wa Malaria Manispaa ya Iringa Dr.Paul Daffa amesema
Kuwa zoezi hilo linalenga kumaliza tatizo la ugonjwa wa malaria katika Manispaa hii.
Daffa amebainisha mada zilizotolewa ni pamoja na majukumu ya Afisa watendaji wa kata na mitaa, na Afisa Afya katika zoezi la uandikishaji na ugawaji wa vyandarua katika kaya.majukumu ya mwenyekiti wa mtaa pamoja na majukumu ya mwanajamii wa kujitolea.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa jumba la maendeleo yanatarajia kumalizika kesho wakati zoezi la usajili litaanza tarehe 24/7 mpaka tarehe 28/7 mwaka huu mara baada ya usajili kukamilika zoezi la ugawaji wa vyandarua katika kaya zote za Manispaa ya Iringa litaanza mara moja.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa