Meya mteule wa Manispaa ya Iringa mh.Ibrahim Ngwada amewaongoza wakazi wa Manispaa ya Iringa kuadhimisha miaka 59 ya uhuru wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya usafi katika eneo la Soko la Kisasa la Mlandege.
Mara baada ya zoezi hilo la usafi Mh.Ngwada alikabidhi vifaa mbali mbali vya usafi kwa Halmashauri ya Manispaa kwa lengo la kuhakikisha Manispaa hii inaendelea kushika nafasi za juu kabisa katika mashindano ya usafi wa mazingira ambayo hufanyika katika Halimashauri zote,miji na majiji Tanzania nzima.
Mh.Ngwada amesema Halmashauri inalo jukumu la kuvilinda vifaa vyote vilivyopo katika Halimashauri na yeye kama msimamizi mkuu wa Halmashauri atasimamia hilo.
Aidha vifaa vilivyotolewa leo ni mifagio ya kawaida 45, buti pea 68,gloves pea 39 kwanja,panga 10 , Torori 5 na Panga 10.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi.Omary Mkangama ameshukuru kwa mh.Meya kutoa vifaa hivyo kwani vitasaidia katika shughuli za usafi katika Manispaa yetu,pia amewataka watumishi wote kushirikiana na madiwani wote ili kuiletea maendeleo Manispaa yetu.
Katika zoezi hilo madiwani, wananchi,wadau,pamoja na tasisi mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira katika eneo hilo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa