Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Iringa kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii imefanya majadiliano na vikundi vya malezi juu ya mkakati wa mawasiniano katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Majadiliano hayo yamefanyika kwa siku tatu katika maeneo tofauti ikijumuisha wadau wa malezi kutokea kata 18 za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
"Serilikali yetu imeleta mpango mkakati wa mawasiliano ambao unawasaidia wananchi kutoa taarifa zinazohusu ukatili wa kujinsia mara moja na kutapatiwa ufumbuzi hivyo basi sisi kama walezi inatuhitaji kuelimisha jamii kuepukana na masuala ya kiukatili"
Akiyasema hayo katika kikao hicho Bi. Mwantumu Dosi ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Iringa ikiwa ni kama chachu ya kuleta mabadiliko dhidi ya ukatili ndani ya Jamii zetu.
Tiniel Mbaga ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa nae amewataka washiriki hao kushirikiana na ofisi yake kwa aina yoyote ya ukatili utakao onekana kufanyika katika Jamii zinazowazunguka kama moja ya njia itakayosaidia kupunguza tatizo hilo
Bwana. Adrian Ngaga kutokea kata ya Mkimbizi ambaye ni mjumbe kwenye kikao hicho amesema jamii zilizo nyingi za kitanzania zimekuwa na tatizo la umasikini hivyo kupelekea mwanamke kuonekana kuathiriwa zaidi kwakuwa waliowengi ni wategemezi kwa wanaume hivyo wakati mwingine kuchochea na kupelekea ukatili kwao.
Aidha ifahamike kuwa, takwimu zinaonesha kwa mwaka 2019 hadi mwezi Juni 2020, Manispaa ya Iringa imeripoti kesi 2761 za ukatili huku 699 wakiwa ni wanaume na
2062 wanawake hivyo ikionesha kuwa wanawake wamekuwa ni wahanga zaidi wa ukatili wakifatiwa na watoto
BAADHI YA UJUMBE ZILIZOTOLEWA KWENYE KIKAO KAMA VIHAMASISHI KATIKA KUPINGA NA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA.
1. Huwezi kuepuka changamoto za maisha kwa ulevi. Kuuwendekeza ulevi ni kuhatarisha maisha yako.
2. Ubakaji ni ushenzi, sio njia ya kupatia utajiri. Acha Tania mbaya
3. Mkiwafundisha watoto wenu watawaheshimu, msipo wafundisha watawaaibisha.
4. Mawasiliano huimarisha uhusiano, jenga Familia zungumza na mwenza wako.
5. Mtoto mwenye tabia njema ni fahari ya ya wazazi, kinyume chake ni huzuni kwa Familia.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa