'Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa fedha kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 45 vya madarasa kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari kwa mwaka 2023."
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake leo tarehe 12/10/2022 kwa lengo la kutoa maelekezo ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba hivyo vya Madarasa kwa Wakuu wa Shule na baadhi ya wakuu wa Sehemu na Vitengo wa Manispaa.
Ngwada amesema jumla ya Shule 14 zitanufaika na ujenzi wa Madarasa hayo ikiwemo Shule ya Sekondari ya Ipogolo madarasa 5,Shule ya Sekondari ya kigungawe madarasa 3,Shule ya Sekondari ya Kihesa madarasa 4, Shule ya Sekondari Klerruu mazoezi madarasa 4,Shule ya Sekondari ya Mtwivila madarasa 5,Shule ya Sekondari ya Shabaha madarasa 3, Shule ya Sekondari ya Mivinjeni madarasa 3 Shule ya Sekondari ya Tagamenda madarasa 3 ambapo kila darasa moja litajengwa kwa thamani ya shilingi milioni 20.
Hata hivyo Mhe. Ngwada ametoa wito kwa wakuu wa Shule kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kabla ya muda ulipangwa wa miezi mitatu na kuwataka kufuata taratibu zote za manunuzi ili kusiwepo na ukiukwaji wa taratibu pia amemtaka Mhandisi kusimamia ubora wa Madarasa yatakayojengwa, uendane na thamani ya fedha iliyotolewa.
Kwa upande wake Tupe kayinga Afisa Elimu Sekondari Manispaa amesema mahitaji ni madarasa 56 hivyo anashukuru kwa kupatiwa madarasa 45 kutoka Serikali kuu kwani imewapunguzia mzigo na kusema madarasa 11 yaliyobaki yatajengwa kwa fedha za Mapato ya ndani.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI MANISPAA YA IRINGA
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa