Waziri wa Maji na Umwagiliaji Engeneir Isack A. Kamwelwe Ameipongeza Manispaa ya Iringa kwa kutatua kero ya upatikanaji wa maji kwa Wananchi wa Mjini na Pembezoni mwa Mji katika Ziara iliyofanyika Manispaa ya iringa siku ya Alhamisi Tarehe 28/12/2017
Aidha Mh, Waziri ametembelea vyanzo mabalimabli vya maji vilivyopo Manispaa ya Iringa ili kujua chanagamoto zinazo vikabili vyanzo hivyo kwa lengo la kushughulikia chanagamoto hizo
Mbali na hayo ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Iringa kuweka ulinzi katika vyanzo vya maji ili kuepuka uharibufu ambao utasababisha kuingia gharama za kutengeneza na kusababisha ukame
Ziara hiyo ilianzia katika wa ukumbi wa Siasa ni Kilimo ambapo imeudhuliwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Mh. Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mh. Ritta Kabati. Mkuu wa Wilaya, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, pamoja na Wataalamu wengine.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa