Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa ikiongozwa na Mwenyekiti Ndg. Abel Nyamahanga waipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi
Hayo ameyasema leo tarehe 19.07.2021 Ndg. Nyamahanga katika ukaguzi wa shughuli na ujenzi wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Aidha miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Nduli, Ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari Nduli, Ujenzi wa Maabara shule ya sekondari Mlamke na Kleruu, Ujenzi wa barabara ya lami ya Kihesa, Kikundi cha vijana mafundi selemala ‘YOUNG FURNITURE GROUP’ cha Mlandege, Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kigungawe, Ujenzi wa jengo la abiria na utawala katika stendi mpya ya Igumbilo pamoja na Mradi wa Machinjio ya kisasa wa Ngelewala
Hata hivyo Ndg. Nyamahanga ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha mradi wa Igumbilo unakamilika na kumtaka kukamilisha suala la ulipaji wa fidia kwa wananchi waliojitolea maeneo yao ili kujengwa kwa stendi hiyo
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndg. Omary Mkangama amesema moja ya sababu iliyopelekea kutokamilishwa kwa malipo ya fidia kwa wananchi waliojitolea maeneo ni kufungwa kwa mfumo wa malipo tarehe 30.06.2021 nchi nzima kwaajili ya zoezi la usuluhishi wa kibenki na maandalizi yakuingia kwenye mfumo mpya wa malipo MUSE ambapo zoezi hilo litakapokamilika ndio Halmashauri itaanza kulipa na wananchi watalipwa baada ya mfumo wa malipo kufunguliwa
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga amemhakikishia Mwenyekiti wa CCM Mkoa kukamilika kwa barabara iendayo katika shule mpya ya Sekondari Kigungawe ambayo imeonekana kuwa na changamoto katika ufikaji kutokea barabara kuu huku Mradi huo ukionesha kusaidia kutatua changamoto na adha ya umbali kwa wanafunzi ambao hapo mwanzo walikuwa wakienda umbali mrefu kufika mashuleni.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa