Manispaa ya Iringa yashika nafasi ya Halmashauri ya tatu (3) katika zoezi la usajili na uandikishaji wa vitambulisho vya matibabu kwa ajili ya wazee wenye umri wa kuanzia miaka 60
Nafasi hiyo imetangazwa na Mkuu wa mkoa wa Iringa Mheshimiwa Ally Hapi katika kikao chake na wazee kilichofanyika ukumbi wa siasa ni kilimo, kwa lengo la kugawa vitambulisho vya matibabu kwa wazee wote ndani ya mkoa wa Iringa.
Aidha Manispaa ya Iringa ilishika nafasi ya tatu (3) kwa kusajili wazee 4261 sawa na asilimia 82%, huku nafasi ya kwanza (1) ikishikwa na wilaya ya mufindi kwa asilimia 113% ikifuatiwa na mji wa Mafinga kwa asilimia 96%.
Kwa upande mwingine Mheshimiwa Hapi amewataka Wakurugenzi na Waganga wakuu wa Halmashauri zote ndani ya mkoa wa Iringa kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matibabu ya wazee na kuwataka wazee kuchukuliwe kama kundi maalumu.
Usajili wa vitambulisho kwa wazee unafanyika Nchi nzima ikiwa ni utekelezaji wa agizo la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Docter John Pombe Magufuli ambapo kimkoa, Mkoa wa Iringa unajumla ya wazee 37196 na waliosajiliwa na kupata vitambulisho vya matibabu ni wazee 30498 sawa na asilimia 81.9%.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa