Mtahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe.Ibrahim Ngwada pichani akikabidhiwa cheti cha ushindi wa pili katika mashindano ya Taifa ya afya na usafi wa mazingira 2022, kundi la Halmashauri za Manispaa Tanzania bara.
Manispaa ya Iringa imepata zawadi ya cheti na fedha kiasi cha tsh milioni kumi ikiongozwa na mshindi wa kwanza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambao wamejipatia kombe, cheti na fedha shilingi milioni 15 na mshindi wa tatu ni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi amboyo imepsta cheti na sh milioni tano.
Tukio hilo la ugawaji wa vyeti na zawadi lilifanywa na Mgeni rasmi Naibu katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt.Seif ShekalagheNovemba 19,2022 Katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwenye kilele cha wiki ya usafi kitaifa na maadhimisho ya siku ya choo Duniani.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa