Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada ametia saini makabidhiano ya maegesho ya vyombo vya moto kutoka wakala wa barabara za Mijini na vijijini (TARURA) ikiwa ni kutii agizo la waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa kuwa vyanzo vyote vya mapato viwe chini ya Halmashauri.
Makabidhioano hayo yamefanyika leo June 30/2022 katika Ofisi ya Mkurungenzi na kuhusisha timu ya menejimenti ya Manispaa ya Iringa na wataalam kutoka (TARURA)ambapo Mstahiki Meya alisisitiza ushirikiano baina ya Manispaa na TARURA kuhakikisha vyanzo hivyo vinaendelea kufanya vizuri katika kukusanya mapato kama ilivyokuwa hapo awali.
Mhe Ngwada amewataka wakusanyaji wa mapato kuwajibika kikamilifu na kusiwepo na upotevu wa mapato katika maeneo yao ya kazi.
Mhe Ngwada amewashukuru TARURA kwa kuwa tayari kutoa msaada wa kitalam pale ambapo watapata changamototo katika kutekeleza majukumu hayo na kusema ataendelea kuwatumia wafanyakazi wale wale kwa kuingia nao mkataba mpya.
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Meneja wa TARURA Mhandisi Makori Kisare amekabidhi Mashine thelasini na sita (36) za kukusanyia mapato (POS) na wafanyakazi kumi na saba ( 17) ambao mkataba wao umeisha tarehe 30/6/2021.
Bw.Makori amesema wako tayari kushirikiana na Manispaa ya Iringa wakati wowote ili kulisukuma gurudumu la maendeleo mbele na kuwa waendelee kufanya kazi na Mhasibu wa TARURA Mkoa wa Iringa Bw Charles Daudi li kuwapa uzoefu katika kutekekeza majukumu hayo mapya.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa