Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia mfuko wa wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu imetoa mikopo ya shilingi milioni 184,734,000/=kwa vikundi vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu katika kipindi cha robo ya tatu Januari hadi Machi 2022.
Akikabidhi hundi hiyo June 15 katka ukumbi wa Mikutano wa Manispaa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe.brahim Ngwada amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutumia fedha walizopata kwa malengo waliyokusudia ili fedha hizo ziweze kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.
Pia amekakabidhi piki piki saba (7) zenye thamani ya shilingi 22,169,000/=katika kikundi cha vijana cha Nguvu kazi kilichopo kata ya Mshindo
Pamoja na Bajai moja yenye thamani ya shilingi 8,500,000/=katika kikundi cha Bajaji Ruaha.
Mhe.Ngwda amewataka kuzitunza pikipiki na bajaji hizo pia kuzingatia urejeshaji wa mikopo hiyo kwa wakati uliopangwa ili na wengine waweze kupata fursa hiyo.
Mwatumu Dossi ni Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa amesema Halmashauri ya Manispaa kupitia mfuko wa wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu imekuwa ikitoa mikopo kwa vikundi vya vijana, kupitia asilimia kumi(10%) ya mapato ya ndani yanayotengwa kwa mgawanyo wa 4:4:2 ambapo asilimia nne inatolewa kwa wanawake,nne kwa vijana na asilimia 2 kwa watu wenye ulemavu.
BI.Mwatum amesema kila Mwaka Idara ya Maendeleo ya Jamii imekuwa ikipokea maombi ya vikundi vinavyohitaji mikopo kutoka kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuongeza ajira.
Aidha Bi Mwatumu amesema katika kipindi cha fedha 2021/2022 kiasi cha Tshilingi 298,829,800/=kilitengwa ikiwa ni mchango wa asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri,ambapo kiasi cha Tshilingi 119,531,920/=kilitengwa kwaajili ya mikopo ya vikundi vya vijana,Tshilingi 119,531,920/=kilitengwa kwaajili ya mikopo ya vikundi vya wanawake, na Tshilingi 59,765,960 kilitengwa kwaajii ya mikopo ya vikundi vya watu wenye ulemavu.
Aidha amesema mikakati iliyopo ya kuimarisha vikundi ni kuendelea kutoa elimu juu ya fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri,kutoa elimu kwa jamii juu ya uundaji wa vikundi,kuendelea kutoa elimu juu ya sifa wanazopaswa kuwanazo wanavikundi wanaohitaji kupata mikopo na kuwaelimisha wanavikundi umuhimu wa kufanya marejesho kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa kikundi cha watu wenye ulemavu ameshukuru kupata mikopo hiyo na kusema Serikali inafanya jambo jema kuwajali watu wenye ulemavu kwa kuwapa mikopo ambayo inawasaidia kuwaongezea kipato.
Katika hafla hiyo ya kukabidhi hundi jumla ya vikundi 26 vya Vijana na vikundi 8 vya watu wenye ulemavu walinufaika na mikopo hiyo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa