Mwanafunzi wa kidato cha tatu Danieli Mwinuka wa Shule ya Sekondari Mkwawa iliyoko ndani ya Manispaa ya Iringa, ameibuka mshindi wa kwanza kitaifa katika shindano la uandishi wa Insha bora kuhusu ubunifu wa majengo na ukadiriaji majenzi.
Shindano hilo imeandaliwa na kisimamiwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Taifa huku likihusisha shule mbalimbali Tanzania bara na Visiwani.
Aidha Mwanafunzi Daniel amepatiwa zawadi ya shillingi 500,000 za kitanzania kama pongezi ya mshindi wa kwanza huku Shule yake ikipatiwa fedha shilingi 300,000 pamoja na vyeti.
Hamid Njovu ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa amesema, anampongeza sana Mwanafunzi Daniel kwa kushinda katika nafasi ya kwanza huku akiipongeza Shule na Walimu kwa jitihada walizozifanya mpaka kupata ushindi huo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Mkwawa ndugu. Adrian Magoyo nae kwa nafasi yake, anawashukuru Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwa kuwashirikisha katika shindano pia ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuwaunga mkono
Sambamba na hilo Mkuu huyo ametoa pongezi za dhati kwa walimu wa masono ya Lugha Mwl. Zedekia Mtega na Azimara Chuma kwa kusimamia zoezi zima la uandishi wa Insha hatimaye kupata ushindi wa kwanza kitaifa.
Daniel Mwinuka ambaye ni mshindi ameleeza kuwa anafurahishwa sana na ushindi huo huku akiwahimiza wanafunzi wengine wajitahidi kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kitaifa watakayoalikuwa kama sehemu yao yakujifunza.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa