Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ,katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Munganno wa Tanzania la kuangamiza viluwi luwi waenezao ugonjwa wa Malaria, Halmashauri Manispaa ya Iringa imetekeleza agizo hilo kwa kupokea viuadudu lita 5,040 vyenye thamani ya Tsh8,970,000/= zilizotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa .
Haya yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya Bi.Mariam Shaibu Mlilapi amezindua unyunyiziaji huo wa viuadudu katika kata ya kihesa Mtaa wa kihesa kilolo na mkimbizi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya akishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Madiwani wa kata mbili zilizohusika, Wataalamu wa Manispaa pamoja na Wananchi.
Lengo la uzinduzi huu ni kuangamiza viluwiluwi ili Sera ya Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia ya Wazee na Watoto chini ya mradi wa mpango wa kudhibiti Malaria wa taifa (NMCP) kuwa ifikapo mwaka 2020, tatizo la malaria nchini liweze kufikia asilimia moja kwa manispaa ya iringa uzinduzi huu wa kuangamiza viluwiluwi umeanza kwa kata mbili ambazo ni gangilonga na kihesa kati ya kata kumi na nane.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa