Dawa, vifaa tiba na vitendanishi Vilivyokwisha muda wa matumizi vimeteketezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa katika eneo la Kihesa Kilolo kwenye dampo kuu la Manispaa chini ya uangalizi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, na mbele ya kaimu RAS DR.Robert Salim.
Akitoa maelezo kabla ya kuanza zoezi hilo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Iringa, Dr. Issessanda Kaniki, amesema dawa hizo na vifaa tiba vinathamani ya shilingi million 249,967,522/= ambazo zilikwisha muda wa matumizi na hazikuwa katika mipango ya vituo, bali zilitolewa na wafadhili mbalimbali.
Kati ya dawa hizo ni dawa za magonjwa ya milipuka nk.
Akitoa ushauri kwa vituo vya afya Dr Robert Salim amesema vituo vya afya vinatakiwa kuhifadhi dawa zake kwa usahihi kwa kuzipanga kwenye mashelfu na sio kuziweka kwenye maboksi ambako zinapata unyevunyevu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa