Kamati ya siasa ya wilaya ya Iringa Mjini imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Manispaa ya Iringa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa kutokana na fedha za tozo za miamala na UVIKO 19 inakamikika kwa muda uliopangwa na yenye ubora.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi( CCM)Wilaya ya Iringa Mjini Ndg. Said Rubbeya, pamoja na wajumbe wa kamati hiyo walitembelea na kukagua miradi tisa (9) ambayo ni pamoja na madarasa, daraja linalounganisha kata mbili, kata ya Mkwawa na Mtwivila pamoja na Kituo cha Afya cha Mkimbizi.
katika ziara hiyo Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa mjini,ndugu. Said Rubbeya ameipongeza Halmashauri kwa hatua nzuri waliyoifikia na ana imani kubwa ifikapo Disemba 15 mwaka huu miradi yote itakuwa imekamilika kama agizo la mhe.Rais Samia Suluhu Hassan alivyoelekeza.
Pia ameupongeza uongzi wa Manispaa kwa usimamizi mzuri kwani baadhi ya miradi tayari imekwisha kamilika hii inawapa imani ya ukamilishaji wa miradi hiyo kwa muda uliopangwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara" lengo la ziara hii ni kuhakikisha uharakishaji wa shughuli ambayo Mhe. Rais mama Samia Suluhu Hassan ametuagiza kuwa ifikapo tarehe 15 Disemba lazima miradi yote iwe imekamilika,,"
Ndugu.Rubbeya, Aliwataka mafundi ambao wamepewa dhamana hiyo ya ujenzi wa miradi kuhakikisha kuwa wanaweka jitihada zaidi ili wakamilishe ujenzi huo kabla ya disemba 15 na wakabidhi tayari kwa madarasa hayo kuanza kutumika maoema januari 2022.
“Chamsingi tumeona kazi inakwenda vizuri na miradi yote thelathini na nne inaendelea vizuri kulingana na muda tulishindwa kutembelea miradi yote lakini ile tuliyoitembelea imetufurahisha.
“Changamoto tulizokutana nazo ni chache na tumeagiza Halmashauri kupitia ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha Kuwa wanazifanyia kazi mapema sana , wengi tuliowapitia wametumia vizuri fedha na fedha”zingine zimebaki alisema Rubbeya.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa