Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy amewataka wataalamu ndani ya Halmashauri ya Manispaa hiyo kuhakikisha wanakusanya mapato ya ndani ipasavyo kwa kuvifikia vyanzo vyote vya mapato.
Ametoa tamko hilo Septemba 4, 2023 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la mwaka 2022/2023 lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
“Tujitahidi kukusanya mapato ya ndani kwa umakini, na kwa kuvifikia vyanzo vvyote vya mapato ndani ya Halmashauri kama tulivyokubaliana ni lazima tukusanye zaidi asilimia 80 ya mapato ya ndani.” Amesema DC Kessy
Aidha, amewaasa wajitahidi kuzingatia matumizi ya fedha kwa uangalifu mkubwa kwani maendeleo ya halmashauri huchangiwa kwa kiasi na mapato ya ndani.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa