Wadau mbalimbali wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Manispaa ya Iringa wametakiwa kutoa Elimu na uhamasishaji wa mapambano dhidi ya UKIMWI, LISHE BORA na UKATILI DHIDI YA WATOTO
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada katika kikao cha wadau hao pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa tarehe 22/11/2022.
Akixungumza na wadau katika kikao hicho Mhe. Ibrahim Ngwada amewakaribisha na wadau hao kufika ofisini kwake muda wowote wakihitaji msaada wa jambo lolote ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na stahiki.
Awali akifungua kikao hicho Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Juli Sawani ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kihesa alisema malengo makuu ya kuwakutanisha wadau hao ni kuondoa muingiliano na mgongano wa kiutendaji na kuomarisha utaratibu wa pamoja wa shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali.
kwa upamde wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Dr.Stephen Ngwale amesema, kuwa Halmashauri imejipanga kuhakikisha inatimiza Diira na Dhima ya Manispaa ya kushirikiana na wadau ambayo inaadhimia kuwezesha utoaji wa huduma bora na endelevu za kijamii na kiuchumi kwa wakazi wake
katika kikao hicho wadau walipewa mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo na kuwapa muongozo wa jinsi taasisi zao zinavyotakiwa kushiriki kikamilifu katika utoaji wa huduma bora kwa jamii hususani utoaji wa elimu juu ya lishe bora, ukatili wa kijinsia pamoja na kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi
Akihitimisha kikao hicho Mhe.Juli Sawani Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa ameshukuru wadau hao kwa ushiriki na kuwatakia utekezaji mzuri katika majukumu yao.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa