Wanafunzi Herman Ngogo na Mary Satiel wa Kidato cha 5 kutoka Shule ya Sekondari Mawelewele iliyopo Manispaa ya Iringa, wameibuka kidedea baada ya kushinda nafasi ya kwanza kitaifa katika shindano la Young Scientists Tanzania kwenye kategori ya Social Science Lililoshirikisha Shule za Sekondari Tanzania bara na visiwani.
Aidha ushindi huo umepatikana kupitia utafiti walioufanya kuhusu mada ya upembuzi wa matokeo ya Elimu bure kwa Elimu Bora ambapo takribani mada 600 ziliwasilishwa na kuifanya mada yao kuwa washindi wa kwanza.
Shindano hilo lilifanyika mwezi Aprili 2020 kwa njia ya mtandao na limekuwa chachu kwa wanafunzi wengine kuongeza juhudi katika masomo yao
Mwl.Haji Abdala ambaye ndie msimamizi wa wanafunzi waliopata ushindi amesema kwa niaba ya walimu wote wa Mawele wele wanashukuru kupata ushindi huo na akibainisha kuwa kwa ushindi wao wamepata zawadi ya fedha kiasi cha shilingi 750,000/= medali,pamoja na vyetii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa amewapongeza wanafunzi kwa ushindi na kusema wametupa fuhari na kuiheshimisha Halmashauri ya Manispaa amesema inaonyesha shule za Manispaa zinaweza kufanya vizuri walimu wajipange kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri zaidi.
Aidha Njovu anesema amejipanga kuweka mazingira ya shule vizuri kwa kuhakikisha wanapata Bwalo pamoja na maabara.
Awali akikabidhi zawadi kwa washindi Afisa Elimu sekondari Bi.Tumpe Kayinga amewataka wanafunzi wa shule ya Sekondari Mawelewele kusoma kwa bidii ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa