Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mhe. Jesca Msambatavangu amewataka madereva bajaji wote wa Iringa mjini kutumia fursa wanazopata katika kazi kuona namna gani wananufaika kiuchumi ili kuzidi kujijenga kimaisha kupitia kazi wanayofanya
Akizungumza leo tarehe 24.02.2021 na madereva bajaji katika ukumbi wa orofea Mhe. Jesca amewataka kufanya kazi kwa juhudi na bidii hata ikiwapasa kujitangaza ili kuzidi kuinua biashara yao, ikizingatiwa Iringa sasa ni eneo mojawapo la utalii lenye kuleta maendeleo hivyo kupitia usafiri wao itaweza kuwanufaisha kwa kuwasafirisha wageni
"Ili kuufikia utajiri mkubwa ni lazima kubadili mfumo wa maisha yaani kujali muda pamoja na kuwa na malengo, hii itatusaidia vijana kuwekeza katika sehemu mbalimbali hata ikiwezekena kujitengenezea akiba ya baadae kuliko kutumia fedha hovyo na kupelekea kutopata faida, inatupasa vijana tujifunze kwa watu waliofanikiwa kwanini, wamefika pale kuliko kuamini imani za kishirikina kama uchawi ambao hauna faida kwa kitu chochote. hivyo juhudi ya mafanikio ni kufanya kazi tu vinginevyo kila kitu utaona ni uchawi na kuishia kulaumu watu" amesema hayo Jesca Msambatavangu
Aidha Mbunge huyo, amewataka madereva bajaji wanapopata changamoto zinazohusiana na vyombo vyao vya usafiri au ushauri wowote wasiache kumjulisha ili kuendelea kusaidia na kutatua shida zinazowakabili maana yeye yupo kwa ajili ya kuwakilisha wananchi wate wa Jimbo la Iringa Mjini
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Iringa (RTO) Yusufu Kamote amewataka madereva bajaji kuzingatia sheria mbalimbali za barabarani ili kijiepusha na adhabu mbalimbali wanazozipata kwakuwa waliowengi wameonekana kutozingatia sheria hizo
Hata hivyo Ndg. Kamote amewaomba madereva bajaji kuthamini kazi zao na kuwa na heshima katika matumizi ya pesa na kuepukana na matumizi holela yasiyo na faida kwao
Aidha madereva bajaji wamemshukuru Mbunge wa Iringa Mjini Jesca Msambatavangu kwa kuandaa kikao kilichowakutanisha na viongozi wa bajaji, viongozi wa serikali pamoja na wadau wa sekta mbalimbali katika kujifunza na kutoa kero na changamoto zinozawakabili huku wakionesha imani kuwa zitafanyiwa kazi pia wakiahidi kuzingatia yote waliyofundishwa hasa kuzingatia sheria za barabarani.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa