Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamefanya ziara ya kutembelea Halmashauriya Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kujifunza namna Halmashauri hiyo inavyotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na mbinu zinazotumika katika ukusanyaji wamapato.
Akizungumza baada ya kutembelea stendi ya mabasi na maegesho ya maroli ya Nyamhongolo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada, ameeleza kuwa safari ya mkoani Mwanza ni kujifunza kwasababu ipo juu katika ukusanyaji wa mapato ingawa Iringa ipo vizuri katika suala la usafi wa mazingira.
“Tunaamini kuja kuona tunaweza kufanya vizuri kwa Manispaa ya Iringa, sisi tunayo stendi ambayo ipo nje ya Mji, tunaanzisha kituo kwa ajili ya malori kwahiyo tunaamini kuja Mwanza kujifunza tumepata kitu kizuri zaidi.” Ameeleza Ngwada
Mhe.Ngwada ameongeza kwa kugusia suala la ukusanyaji wa mapato katika Halmashaurizote mbili;
“Hapa Ilemela mapato yapo zaidi ya Bilioni 11 lakini sisi Iringa mapato yetu yalikuwa zaidi ya Bilioni 4 na sasa hivi tumekusudia kukusanya zaidi Bilioni 6 na tunaamini kwa yale ambayo tumeyaona hapa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mapato, yetu tutaenda kuyaongeza.”
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Dkt. Godfrey Mbagali, ameeleza kuwa Iringa inajivunia kuwa na Halmashauri safi na mwaka 2023 kwa kuwa wa 3 ngazi ya Manispaa.
“Tumegundua vyanzo vingine vya mapato, sisi tulikuwa hatuna chanzo cha kupakia na kushushamizigo, pia kuna mahakama inayotembea na sisi utamaduni huu tutaenda kuanzisha kwetu ili watu wote wawe wanalipa kodi na waone kulipa kodi ni fahari.”
Dkt.Mbangali ameongeza kwa kuwaalika viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa lengo la kujifunza na kufanya utalii wa ndani kwa Nyanda za Juu Kusini;
“Tumejifunza kuwa wale wanaozalisha taka nyingi wana kiwango chao cha kulipa ushuru vilevile wanaozalisha taka chache, kwahiyo tuna vitu vingi tumejifunza nanyi mje kwetu mjifunze mazuri na uwekezaji tulionao na kwa sasa tunaendelea na utalii wa Nyanda za Juu Kusini.” Ameeleza Dkt. Mbangali.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa