Mbunge wa Iringa mjini Mhe. Jesca Msambatavangu ametoa jumla ya mifuko 150 ya saruji kwa Shule za Msingi Ipogolo na ya Mawelewele ili kukamilisha ujenzi wa madarasa
Mifuko hiyo imetolewa siku ya tarehe 9.01.2021 na Mbunge huyo alipokuwa akifanya ziara yake ya kuangalia maendeleo ya miradi hiyo ambayo kukamilika kwake kutapunguza changamoto ya madarasa kwa wanafunzi, alisema Mbunge huyo
Aidha Shule ya Msingi Ipogolo ilipata Mifuko 100 huku Shule ya Msingi Mawelewele kupata mifuko 50
Akizungumza kwa nyakakati tofauti akiwa akikabidhi mifuko hiyo amesema kuwa, lengo lake ni kushiriki katika kuchochea maendeleo kwenye sekta ya elimu ndani ya Manispaa ya Iringa akiwa kama mmoja wa wadau wa elimu
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa